You are currently viewing SKENDO ya Dola milioni hamsini zilivyoibwa toka Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Mwinyi

SKENDO ya Dola milioni hamsini zilivyoibwa toka Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Mwinyi

SMZ kwa maelekezo ya Mwinyi wamefungia tovuti yetu zanzibarleaks.com na huipati ukiwa Zanzibar hadi utumie VPN. Sisi ni sauti ya vilio vya Wazanzibari wanaoteseka na ufisadi wa kutisha wa serikali hii.Endeleeni kutufungia lakini hatutachoka kuisemea Zanzibar yetu kwani hii ni kazi ya Allah!!

Kuna wizi mwingine huu hapa… zaidi ya dala za kimarekani milioni hamsini hiyo kama shiling bilioni 125 zimeibwa toka Zanzibar miaka miwili iliyopita na Rais Mwinyi anajuwa mana kashiriki. Waliosuka mpango wakishirikiana naye walisema kuna mradi wa barabara na walitaka hiyo pesa kama bank guarantee basi wakapewa! Mradi ukawa hewa pesa ikawekwa benki ya Standard Chartered na haikurudishwa Zanzibar.baadaye wakaunda stori kwamba imewekezwa nchi za nje kwa niaba ya Wazanzibari kupitia kampuni ya Mauritius 😭😭😭😭
Wote huo wanafanya ulikuwa wizi. Kikundi cha Rais Mwinyi kikaweka hizo pesa kwenye sarafu za mtandao wanaita cryptocurrency wakacheza michezo na wagenge ya wasafisha hela wa dunia pesa ikapelekwa Marekani! Sasa si mwafahamu wachawi huwa wanakosana wenyewe kwa wenyewe basi partner mmoja walifanya naye hiyo dhulma kwa Wazanzibari anataka shea yake ndo sasa wanazozana kumpa. Mwinyi yeye kenda Marekani kimya kimya mkicheki picha za vikao vya CCM leo hayupo.Kule Marekani kamweka kijana wake anaenda kumnunulia jumba Los Angeles kwa fungu lake kwenye hizo bilioni 125!!Sisi zetu dua Wazanzibari Inshallah tutaona kama utadumu hapo maisha yako yote na kama utazikwa navyo kwa dhulma inazopitia Zanzibar hii.Tuna watu hawana dawa mnazi mmoja hapo hatua chache toka Ikulu lakini una Rais anaiba kwenda mnunulia mwanaye nyumba Marekani!

Shirikisha