You are currently viewing Utafiti wa Democrarcy Group ya Marekani waonesha Hussein Mwinyi hana uwezo wa kushinda Urais Zanzibar 2025

Utafiti wa Democrarcy Group ya Marekani waonesha Hussein Mwinyi hana uwezo wa kushinda Urais Zanzibar 2025

Shirika linalojihusisha na kutoa ushauri wa uchaguzi la nchini Marekani, The Democracy Group, limesema kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hussein Mwinyi angepata asilimia 20 tu ya kura zote kama uchaguzi mkuu wa Zanzibar ungefanyika mwezi Oktoba 2023. Shirika hilo limesema katika ripoti yake kwenda kwa Sekretariati ya Chama Cha Mapinduzi kuwa utafiti wake umegundua kuwa tuhuma za rushwa zinazomkabili Rais Mwinyi ni chanzo cha kukosa uhalali wa uongozi visiwani Zanzibar. Hata hivyo, ripoti ya kampuni hiyo imesema kuwa Rais Mwinyi anajiandaa kuomba ridhaa ya kuteuliwa na CCM kugombea urais wa Muungano mwaka 2025. Chama Cha Mapinduzi kimelipa shirika hilo kazi ya kufanya utafiti kuhusu changamoto mbalimbali za kisiasa visiwani Zanzibar.

Kwa taarifa zaidi kuhusu utafiti wa awali wa shirika hilo, pakua ripoti yao hapa.

zanzibar2025

 

Shirikisha